HAPPY NEW MONTH OF MAY
- 01
- May

💥HAPPY NEW MONTH OF MAY💥
Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu.
HERI YA MWEZI MPYA WA TANO.
Ndugu, Tunapoanza mwezi huu wa tano naomba nikushirikishe ujumbe huu muhimu Sana kwako;
Tupo katika nyakati za siku za mwisho ambazo Yesu anakaribia kurudi kulichukua Kanisa lake.
KANISA NI NINI??
✓ Kanisa ni Mwili wa Kristo – 1Korintho 12:27
✓ Kanisa siyo jengo bali ni mimi na wewe
tunaomwamini na kumtii Bwana Yesu – 1Korintho 6:19
✓ Kanisa ni wale wote wanaomwamini na kumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao (Waliookoka) – Warumi 10:9-10
✓ Kanisa ni wale waliohamishwa kutoka katika ufalme wa shetani na kuingizwa katika Ufalme wa Mungu – Wakolosai 1:13 .
Wakati tunasubiri Yesu arudi KULINYAKUA Kanisa lake UAMSHO lazima kwanza utokee.
UAMSHO utasababishwa na UFUNUO KUHUSU UFALME WA MUNGU. katikati ya UAMSHO Yesu atarudi kulichukua Kanisa lake.
UFUNUO KUHUSU UFALME WA MUNGU UTASABABISHA –-> UAMSHO WA KANISA –-> UNYAKUO WA KANISA
Katika nyakati hizi za mwisho ujumbe utakao hubiriwa sana kwa UFUNUO WA MUNGU ni ujumbe wa Ufalme wa Mungu.
Luka 8:10 “Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua SIRI ZA UFALME WA MUNGU; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe”.
UHUSIANO ULIOPO KATI YA INJILI YA UFALME WA MUNGU NA NYAKATI ZA MWISHO.
Mwisho wa dunia hautegemei majanga au matukio bali ni pale UFUNUO WA HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU Utakapohubiliwa kwa kila taifa na kwa kila kiumbe.
Tena HABARI NJEMA YA UFALME itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; HAPO NDIPO ULE MWISHO UTAKAPOKUJA.
MATHAYO 24:14
And THIS GOSPEL OF THE KINGDOM will be preached in the whole world as a testimony to all nations, and THEN THE END WILL COME.
MATTHEW 24:14
Kwenye kiingereza anasema THIS GOSPEL OF THE KINGDOM anatumia neno “THIS” akimaanisha ya kwamba zipo injili za aina mbali mbali zinazohubiliwa lakini injili ya UFALME
itakapoubiliwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; HAPO NDIPO ULE MWISHO UTAKAPOKUJA.
NDUGU, MUNGU AMENIFUNULIA SIRI ZA UFALME WAKE NA KUNIPA JUKUMU / KAZI YA KUHUBIRI NA KUFUNDISHA INJILI YA UFALME WA MBINGUNI NA KUHAKIKISHA KILA MTU ALIYEKUSUDIWA NA MUNGU ANAINGIA KWENYE UFALME WA WAKE.
NIMEWEKA WAZI NDOTO YA UFALME WA MUNGU KWANZA-UMK ILI KILA AISOMAYE APATE UFAHAMU. Habakuki 2:2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
Fungua hiyo link ya tovuti hapo chini Kwa maelezo zaidi Kuhusu Ufalme wa Mungu Kwanza – UMK
👇👇👇👇👇
www.aar.co.tz/umk
KARIBU TUUJENGE MWILI WA KRISTO.
© MCHUNGAJI NA MWALIMU
© Dawson. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza (UMK)
© Kingdom Influence Network
© All Around Rest (AAR)
© www.aar.co.tz/umk
© www.aar.co.tz
© 0714 606 500
© 2 Nyakati 15:15
© Mathayo 6:33
© Isaya 42:6-7
© U M K
© A A R
Follow Us
Mafundisho
- UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
- HAPPY NEW MONTH OF MAY
- HIKI NDICHO AMBACHO DEMOKRASIA INAFANYA KWENYE NCHI YA MUNGU.
- MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
- UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu),
UMK Forums
Recent Posts
-
-
Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na usafirishaji.
Tujadili Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na...
By dawson , 1 month ago