MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
- 30
- Apr

Nikasikia mahali, mama mmoja amemsahau mtoto wake mchanga wa miezi sita kwenye benchi eti anakimbia kuwahi rejesho la mkopo, nikasema huu nao ni ugonjwa wa akili.
Tunao wagonjwa wengi sana wa akili tunaishi nao, na haya magonjwa ya akili yanasababishwa na kuibebesha mioyo yetu mizigo mizito inayosababisha msongo wa mawazo (Stress).
Nyuso nyingi za watu zinaonesha tabasamu na furaha lakini mioyoni mwao wamebeba huzuni nzito na mambo mazito.
Watu Wana maumivu makali Sana kwenye mioyo yao, lakini wanaigiza kuwa na nyuso za furaha na tabasamu.
Watu wanatembea na maumivu makali Sana kwenye mioyo yao, wengine ni viongozi wetu wakubwa tunaowategemea kwenye maendeleo ya nchi, wengine ni watu tunaowategemea kwenye maendeleo yetu binafsi.
Hata wengine wanatumia vileo kama pombe na sigara kutafuta amani ya moyo, wengine wanatembea nje ya ndoa zao kutafuta furaha lakini hawaipati.
Tunaishi maisha ya kuigiza, tumekuwa na wagonjwa wa akili wengi Kwa sababu tumeibebesha mioyo yetu mambo yasiyostahili.
Presha, vidonda vya tumbo, msongo wa mawazo vimekuwa ni sehemu ya maisha ya watu wengi.
Kuna watu tunafikiri wanaweza kutusaidia, tunawakimbilia kutafuta msaada kwao, kumbe na wao Wana ya kwao yanayowasumbua, nao wanahitaji msaada.
Nilikutana na mama mmoja ana nyumba ya kifahari na gari la kifahari lakini ana mateso makubwa Sana, nikakutana na kijana mmoja ana kazi nzuri tu, lakini ana msiba mkubwa Sana unaomsubua, Nikakutana na kiongozi mkubwa wa serikali analia kama mtoto maana mambo yamemlemea.
Yule unayemtegemea na unafikiri anaweza kukusaidia katika msiba ulio nao, na yeye ana msiba wake unaomsumbua, na yeye anatafuta msaada ila hajakwambia.
YESU ANATOA WITO KWA WATU WOTE
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
MATHAYO 11:28
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. WAFILIPI 4:6-7
Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
MATHAYO 6:31-33
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
AYUBU 22:21
SOTE TUNAHITAJI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU ILI TUPATE UTULIVU WA MIOYO YETU, MAANA KWENYE UFALME WA MUNGU NDO KUNA MAISHA YETU NA MAHITAJI YETU.
KAMA MAISHA YA SAMAKI KWENYE MAJI NDO MAISHA YA MWANADAMU KWENYE UFALME WA MUNGU.
Usisahau kupata nakala yako ya kitabu cha “MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAFAHAMU KUHUSU SERIKALI YA UFALME WA MBINGUNI”,
Kitabu hiki kinapatikana; Kwa mkoa wa Kagera kinapatikana katika Kanisa la Rhema Outreach Ministries lililoko Bukoba Mjini Mtaa wa Miembeni,
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam tembelea duka la vitabu la House of Wisdom Bookshop lililoko Posta au Duka la vitabu la Kanisa la Winners Chapel Banana Ukonga.
Pia tunaweza kuwasiliana +255 757 263 226.
*© Dawson. R. Kabyemela*
*© Ufalme wa Mungu Kwanza*
*© All Around Rest*
*© 2 Nyakati 15:15*
*© Mathayo 6:33*
*© 0714 606500*
*© U M K*
Follow Us
Mafundisho
- UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
- HAPPY NEW MONTH OF MAY
- HIKI NDICHO AMBACHO DEMOKRASIA INAFANYA KWENYE NCHI YA MUNGU.
- MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
- UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu),
UMK Forums
Recent Posts
-
-
Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na usafirishaji.
Tujadili Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na...
By dawson , 1 month ago