Home » Mafundisho » NILIMUONA MUNGU ANAWATAZAMA WANADAMU ANACHEKA

NILIMUONA MUNGU ANAWATAZAMA WANADAMU ANACHEKA

NILIMUONA MUNGU ANAWATAZAMA WANADAMU ANACHEKA

Nikashangaa sana na kujiuliza Kwa nini??,

Wakati ninashangaa na kujiuliza  maswali nikasikia sauti ikiniambia; 

“Kwa sababu tunatengeneza matatizo wenyewe halafu tunataka kutatua hayo matatizo Kwa njia zile zile, mifumo Ile Ile, watu wale wale na Kwa akili zile zile zilizosababisha hayo matatizo.”

Zaburi 2:4

Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

Mungu akitazama jinsi wanadamu tunavyohangaika na kutapatapa na maisha katika dunia yake anacheka.

Tambua hii Dunia na Kila kilichomo ndani yake ni program (Application software) ya Mungu.

Zaburi 24:1 

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Kama Dunia hii na Kila kilichomo ni product ya Mungu, basi Kuna vigezo na msharti ya kuzingatia ili kuweza kufanikisha maisha yetu katika hii dunia.

Isaya 1:19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

KUMTII MUNGU NI UFUNGUO WA MAFANIKIO (Baraka za Mungu zimefungwa kwenye Kutii Neno lake).

WITO WA MUNGU KWA WATU WOTE NI;

MATENDO YA MITUME 17:30 

“Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza WATU WOTE WA KILA MAHALI WATUBU.”

MATHAYO 3:2 

TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

MATHAYO 4:17 

Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

MATENDO YA MITUME 2:38 

Petro akawaambia, TUBUNI mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

KUTUBU MAANA YAKE NI KUACHA MIFUMO YA KIDUNIA NA KUKURUDI KWENYE MFUMO WA UFALME WA MUNGU.

UFALME WA MUNGU NI ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.

Usisahau kupata nakala yako ya kitabu cha “MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAFAHAMU KUHUSU SERIKALI YA UFALME WA MBINGUNI”, 

Kitabu hiki kinapatikana; Kwa mkoa wa Kagera kinapatikana katika Kanisa la Rhema Outreach Ministries lililoko Bukoba Mjini Mtaa wa Miembeni,

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam tembelea duka la vitabu la House of Wisdom Bookshop lililoko Posta au Duka la vitabu la Kanisa la Winners Chapel Banana Ukonga. 

Pia tunaweza kuwasiliana +255 757 263 226.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *