UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu),
- 30
- Apr

Ukikutana na samaki nchi Kavu Kuna mawili; Awe anatapatapa au amekufa, kwanini? Kwa sababu nchi Kavu siyo mazingira yake aliyoumbiwa kuishi.
Ukikutana na Mwanadamu nje ya UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu), Either anahangaika na kutapatapa ama amekufa. Ndo maana Yesu alimwambia Yule kijana waache wafu wawazike wafu wao.
Tunahangaika kutafuta msaada nje ya mazingira yetu tukifikiri tutafulu.
Nimeona watu wakihangaika na kutapatapa wakitafuta msaada wa kutoka katika changamoto mbali mbali za maisha.
Kuna watu tunajaribu kuwasaidia nje ya UWEPO WA MUNGU/ Edeni ( ufalme wa Mungu ) na tunashindwa.
Maisha ya samaki na mahitaji yake yote, yapo kwenye maji.
Maisha ya mwanadamu na mahitaji yake yote yapo kwenye Uwepo wa Mungu (Edeni / Ufalme wa Mungu).
MATHAYO 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Maisha ya mmea na mahitaji yake yote yapo kwenye ardhi.
Maisha ya nyota na mahitaji yake yote yapo angani.
USIHANGAIKE KUTAFUTA MAISHA HANGAIKA KUTAFUTA UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu – Your Place and position In the kingdom) NDO ULIPOTEZA.
Msaada wa Kwanza wa kumsaidia samaki aliyeko nchi Kavu ni kumrudisha majini na siyo vinginevyo.
Msaada wa Kwanza kwa mwanadamu anayehangaika na kutapatapa ni kumrudisha kwenye UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu ).
Tunza mazingira ya UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu ) NAYO YATAKUTUNZA.
Usisahau kupata nakala yako ya kitabu cha “MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAFAHAMU KUHUSU SERIKALI YA UFALME WA MBINGUNI”,
Kitabu hiki kinapatikana; Kwa mkoa wa Kagera kinapatikana katika Kanisa la Rhema Outreach Ministries lililoko Bukoba Mjini Mtaa wa Miembeni,
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam tembelea duka la vitabu la House of Wisdom Bookshop lililoko Posta au Duka la vitabu la Kanisa la Winners Chapel Banana Ukonga.
Pia tunaweza kuwasiliana +255 757 263 226.
*© Dawson. R. Kabyemela*
*© Ufalme wa Mungu Kwanza*
*© All Around Rest*
*© 2 Nyakati 15:15*
*© Mathayo 6:33*
*© 0714 606500*
*© U M K*
Follow Us
Mafundisho
- UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
- HAPPY NEW MONTH OF MAY
- HIKI NDICHO AMBACHO DEMOKRASIA INAFANYA KWENYE NCHI YA MUNGU.
- MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
- UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu),
UMK Forums
Recent Posts
-
-
Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na usafirishaji.
Tujadili Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na...
By dawson , 1 month ago