UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
- 02
- May

MATHAYO 6:33
Bali utafuteni kwanza UFALME WAKE, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
- Ufalme wa Mungu ni Mfumo wa utawala uliobeba uwepo wa Mungu Kwa misingi ya Haki, Furaha na Amani katika Roho Mtakatifu.
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. WARUMI 14:17
- Ufalme wa Mungu ni Mazingira yenye na yaliyobeba Uwepo wa Mungu (Bustani ya Edeni)
BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
MWANZO 2:15
- Ufalme wa Mungu ni ushawishi wa Mungu unaotawala juu ya eneo lake, akiweka mapenzi yake, kusudi lake na nia yake, kuzalisha raia na watu wanaoelezea utamaduni wake na kuakisi asili yake.
Ufalme huathiriwa na akili ya mfalme sio sheria ya kundi la watu, ndio maana Yesu alisema ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe duniani kama huko mbinguni. MATHAYO 6:9-10
- Ufalme wa Mungu ni Roho Mtakatifu ndani yetu.
wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. LUKA 17:21
Ndugu usiache kuomba Ufalme wa Mungu uje katika Kila eneo la maisha yako maana huo ndiyo Mfumo wa mafanikio yetu.
Kama vile samaki ambavyo hawezi kufanikiwa nje ya maji vile vile na Wewe huwezi kufanikiwa nje ya Ufalme wa Mungu.
NITAELEZA ZAIDI KWENYE VIDEO ZINAZOKUJA. USIACHE KUFUATILIA.
Ubarikiwe na Bwana Yesu.
© MCHUNGAJI NA MWALIMU
© Dawson. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza (UMK)
© Kingdom Influence Network
© All Around Rest (AAR)
© www.aar.co.tz/umk
© www.aar.co.tz
© 0714 606 500
© 2 Nyakati 15:15
© Mathayo 6:33
© Isaya 42:6-7
© U M K
© A A R
Follow Us
Mafundisho
- UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
- HAPPY NEW MONTH OF MAY
- HIKI NDICHO AMBACHO DEMOKRASIA INAFANYA KWENYE NCHI YA MUNGU.
- MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
- UWEPO WA MUNGU (Edeni / Ufalme wa Mungu),
UMK Forums
Recent Posts
-
-
Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na usafirishaji.
Tujadili Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji wa madini na...
By dawson , 1 month ago